Текстов песен в базе: 1 278 222
Kemosabe

Kemosabe

Fid Q

Текст песни

Niliamini mapene hayatoshi. na niki-hustle siyakosi/
Sababu. sipo kwenye loss na life simple huwa hai-cost/
Kwahivyo nikaenda Dar na treni… of thoughts./
Sikwenda kuzubaa au kushangaa nikusaka chapaa boss/
Sikutaka kuivaa mikosi. nilitaKa kuivaa mikoti/
Sikuwa na passport.password. pin. lakini ni crack codes/
Walionisapoti wote siwaoni kwa line/
Wakini-approach ili nifungue pochi ya noti tu-shine.hatuko fine/
Je mimi ni kaka mubaya??? kaka aso haya./
KAKA. huniitaga NAKAAYA/
Mama C huniita brother bila shaka. Mozaya/
Niko sick & tired of being sick & tired/
Na huu ni mwaka wa ndui/ Sitaki upele urudi tena. mnachotaka sikijui/
Nashukuru hamtopata mbawa ikiwa mtaupata huo uchui/
Mnautaka uadui? mnayempaka ni mtata. makaka hamkui?
Mmeendekeza hila. legeza hasira za harakati/
Mie nita-ball… hata kwa mpira wa makaratasi/
Unaweza ukahisi mie napita tu. kwakusahau mie nina-hustle/
Nimezaliwa Afrika. ugumu wa maisha umenifunza ku-struggle/
Ukiwa idle. unamu-attract shaytwan (SHETANI)/
Kichwani nina MSAHAFU na BIBLE. life ni zaidi ya ku-have fun/
Kwani. Kila kicheche anajiona ni mzima/
Na njia pekee ya kuepuka ngoma ni kugoma kupima/
Ikiwa maujuzi haya hayakugusi. itanilazimu nikuelewe/
Sometimes hata kamusi. huimiss tafsiri yenyewe/
Nalindwa na dua za mama. tangu baba simjui/
Namfanya adui mwenye njama aache drama na akue/
Ili ajijue kabla hajakwama huko mrama asitue/
Ajikwamue kwenye lawama. yenye maana yamchukue/
Kisha anaiombee mimi ili nifaidike kwa hizi mbio/
Siamini kwenye umasikini hivyo sihofii mafanikio/
Ndiyo. mie ni LEO kwahiyo sifikirii kushindwa/
Zingatia kauli hiyo hausikii inaashiria ubingwa?/
Mie ni mbishi. muulize Nikki — hatopinga/
Na hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka la simba.
Поделиться ссылкой:
Короткая ссылка: https://tekstpesni.ru/s/5bUJ

Тексты других песен исполнителя

© 2017–2025 Тексты песен
Все тексты песен на сайте размещены пользователями, редакцией или собраны из открытых источников.
При копировании материалов ссылка на сайт обязательна.
Связаться
Уважаемые обладатели прав на музыку! На сайте не выкладывается музыка, ее нельзя скачать, послушать и тому подобное.