Ah Leo Chereko Chereko
Mwanenu nimekuwa
Zile kuringa mideko itapungua
Ahsante mama ulinifunza nkajua
Baba kasema kuomba mwiko
Raha ya chumvi kununua
Tena si kwa nazi
Si hirizi za waganga
Kwa baraka za baba na mama
Tu na dua
Waambie paparazi
Pingamizi wenye viranga
Waliosema hayawi hayawi yamekuwa
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana
Ooh. Ndoa baraka
Ukipata ushukuru
Maana wanayoililia ni wengi sana
Kwetu talaka
Kuitoa ni kufuru
Nimefunzwa vumilia
Niushinde ujana
Ili kesho mahususi
Kusudi wasinong’one
Embu nichumu niringe washushuke
Na hii pete ya harusi
Nakuvisha waone
Wakale sumu
Wavimbe wapasuke
Ati nashika nanga
Nteke nsichomoke ndani (Anameremeta)
Futa namba wablock vimada wa zamani (Anameremeta)
Sio vijembe vya kanga waziwazi mambo hadharani (Anameremeta)
Waliopanga mwenye nyumba kaja ndani (Anameremeta)
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (Oh, kwaheri baba mama)
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana
Imefika tamati
Tulisubiri kitambo
Leo samaki
Kanasa kwenye chambo
Pongezi kwa kamati
Yanavutia mapambo
Napata picha safi
Litanikoma bundle
Mwanamke usafi
Gaga kulisugua
Mume akirudi sharti
Viatu kumvua
Kitandani marashi
Massage kumchua
Kisha anza sayansi
Viuno kutengua
Mambo ya kuzima taa
Si mahaba ni kuwanga
Washa japo ka mshumaa
Mumeo aone shanga
Makeup kinanda
Kaka suit kama mbunge (Anameremeta)
Mulo changa muda kujipooza na punje (Anameremeta)
Momo ndani Shivo amekuja na Fumbwe (Anameremeta)
Kula chanda ukishiba ruksa kafunge (Anameremeta)
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (Eh, kwaheri baba mama)
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana
Saa nataka kusasambua (Sasambu)
Me nasasambua (Sasambu)
Aby Dad nasasambua mimi (Sasambu)
Sasambua
Tuone
Mguu moja juu (Sasambu)
Usishushe chini (Sasambu)
Cheza jitazame (Sasambu)
Sasambua
Tuone
Aisha kimobitel (Sasambu)
Nipe za baloteli (Sasambu)
Nyonga kibaiskeli (Sasambu)
Sasambua
Tuone
Akaa kama unashika ukuta (Sasambu)
Ifanye unashusha (Sasambu)
Taratibu zungusha (Sasambu)
Sasambua
Tuone
Sasambu! Sasambu! Sasambu!
Sasambua
Tuone
Kama unawasha bajaji (Sasambu)
Imwagie na maji (Sasambu)
Tuwakomeshe vizazi (Sasambu)
Sasambua
Tuone