Текстов песен в базе: 1 278 356
Yote Sawa

Yote Sawa

Nandy

Текст песни

Mimi sio kama wale
Walopita zamani mpenzi
Ooh niamini mwendo uwe sare
Usije nicha njiani mpenzi
Kule niliona mazito
Penzi lilikuwaga la mpito
Kulalama kulichosha koo
Ila nashukuru ilinikomaza roho
Licha ya kuitoa mchangani
Sikuacha kujipa imani
Japo mengi yalinikata maini
Nikaliwazua na msondona
Uzuri haupotei ramani
Ubaya hauvaishwi miwani
Nikachoka madongo ya gizani
Na mateso ya Sodoma
Yote sawa, mapenzi mboga nachaja jamaa
Yote sawa, nimeshapata shuruba yakaniumiza
Yote sawa, wouuh
Yote sawa (Yote sawa)
Tafsiri ya penzi sio kitanda tu
Ina mengi juu yake ni mapenzi
Sio kama sioni na sio ushamba boo
Kuna wengi niwafuate
Nilijaribu nilipoweza kufanya
Haikuonekana kwangu ikawa aibu
Kunichombeza kwa sana kumbe ananidanganya
Licha ya kuitoa mchangani
Sikuacha kujipa imani
Japo mengi yalinikata maini
Nikaliwazua na msondona
Uzuri haupotei ramani
Ubaya hauvaishwi miwani
Nikachoka madongo ya gizani
Na mateso ya Sodoma
Yote sawa, mapenzi mboga nachaja jamaa
Yote sawa, nimeshapata shuruba yakaniumiza
Yote sawa, wouuh
Yote sawa (Yote sawa)
Поделиться ссылкой:
Короткая ссылка: https://tekstpesni.ru/s/6Nf2

Тексты других песен исполнителя

© 2017–2026 Тексты песен
Все тексты песен на сайте размещены пользователями, редакцией или собраны из открытых источников.
При копировании материалов ссылка на сайт обязательна.
Связаться
Уважаемые обладатели прав на музыку! На сайте не выкладывается музыка, ее нельзя скачать, послушать и тому подобное.